Endapo unahitaji kupata mkopo kutoka EBS FINANCE, baada ya kuwa umewasiliana na ofisi yetu na kuwa na dhamana inayoweza kukupatia mkopo, unaombwa kufika ofisini ukiwa na dhamana yako na kitambulisho chako. Dhamana yako itapokelewa na kufanyiwa ukaguzi ili kutambua thamani yake kwa bei ya sokoni kisha itafahamika ni kiasi gani cha mkopo utapata, Mkataba utaandaliwa na baada ya kusaini, utakabidhiwa mkopo wako. Kufuatia masharti na vigezo vyote kuzingatiwa, utapata mkopo siku hiyohiyo ndani ya saa moja tu.
Aina za iPhones zinazokubalika ni kuanzia iPhone X mpaka iPhone 13 Pro Max, kwa kutegemea na mchanganuo unaopatikana hapa kuhusu kiwango cha mkopo kinachoweza kutolewa baada ya tathmini ya dhamana.
EBS Finance inakubali aina tofauti za laptop, zilizo katika ubora na ni za matoleo ya miaka ya karibuni. Tutatathmini bei yake ya sokoni na kutoa mkopo kutegemeana na thamani yake. Laptop itafanyiwa uchunguzi kuhakiki hali/ubora wake.
Ebs Finance inakubali aina zote za magari ambayo yapo katika hali nzuri na ni ya matumizi binasi na yana namba za usajili kuanzia C. Gari itatathminiwa kwa bei zilizopo sokoni na mkopo utakabidhiwa kwa kutegemea thamani yake. Magari yanayokubaliwa ni kama IST, BMW, Spacio, Crown, Rangerover, Hilux na mengine mengi ikiwemo ya Toyota na ya UK. Gari litafanyiwa uchunguzi kuhakiki hali/ubora wake.
Kampuni ya EBS Finance, inatoa mikopo kuanzia TZS 500,000/= kama kiwango cha chini mpaka kiwango ambacho kinategemea thamani ya dhamana yako. Uchanganuzi utafanywa ili kutambua thamani ya dhamana yako katika bei za sokoni.
Kampuni ya EBS Finance inatoa mikopo ya muda mfupi, mikopo ya dharura, yote hio kwa muda wa miezi mitatu tu.