EBS Finance Company Limited ni kampuni ya mikopo ya Tanzania ambayo inafanya kazi ya kutoa mikopo ya dharura ikiwa na makao makuu yake Dar es salaam kama mahali ilipoanzishwa. Kwa sasa ina matawi mawili mengine ikiwa ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro na wa Arusha. Kampuni inatarajia kupanua huduma zake kwenda mikoa yote ya Tanzania na nje ya Tanzania.
Wataalamu wetu hapa EBS Finance wanatoa wigo wa upatikanaji wa mikopo kusaidia watu binafsi, biashara ndogo, za kati na kubwa katika jamii ya Tanzania na duniani kote.
Dhumuni letu ni kuhakikisha changamoto ya dharura ya kifedha inayowakumba watu wengi, biashara na makampuni hapa Tanzania inafika mwisho kwa kuwa na uhakika wa kupata msaada wa kifedha mara moja ndani ya lisaa tu.
Kampuni ya EBS Finance inatoa huduma ya mkopo wa dharura kwa kutumia vitu vinavyohamishika ambavyo vitaletwa ofisin kwetu kama vile simu aina ya IPHONE (kuanzia iphone X), kompyuta mpakato (aina tofauti) na magari (binafsi yaliyo katika hali nzuri). Unatakiwa kuwa na vitu vilivyotajwa na kadi yako ya uraia (NIDA, au Pasipoti au leseni ya udereva) ili kuweza kupata mkopo.
Timu ya Menejimenti na Mikopo
Timu ya Utaalamu na Tathmini ya Hatari